Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Nyasa Big Bullets dhidi ya Yanga umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Yanga ikisheheni nyota wengi kutoka kwa kikosi cha U20, iliwapa wakati mgumu Nyasa Big Bullets ambayo walitumia kikosi chao cha kwanza kusaka ushindi katika mchezo huo wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi
Kocha Said Maulid amewapongeza vijana wake kwa kuonyesha mchezo mzuri licha ya kutokuwa na uzoefu katika mechi za Kimataifa
Nyota wa kikosi cha kwanza walioshiriki mchezo huo ni Metacha Mnata, Joyce Lomalisa, Clement Mzize, Chrispine Ngushi na Denis Nkane ambaye hata hivyo alipata majeraha na kulazimika kupatiwa matibabu ya dharura
Waganda Moses Aliro na Sharifu Kimbowa ambao wapo Yanga kutoka klabu ya Wakiso Fc kwa makubaliano ya ushirikiano, walishiriki mchezo huo uliochezwa kwa dakika 70 kila kipindi kikichezwa dakika 35
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
No comments:
Post a Comment