Haji Manara awalipua Simba baada ya Mkude kutua Yanga, atoa masharti haya - EDUSPORTSTZ

Latest

Haji Manara awalipua Simba baada ya Mkude kutua Yanga, atoa masharti haya

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Baada ya Jana Julai 12 Klabu ya Yanga kutangaza kumsaini Kiungo Jonas Mkude aliekulia katika Klabu ya Simba SC.


Ile kauli ya Simba kutaka kumuaga mchezaji huyo kwa heshima ni kama inaonekana kuwa ngumu hivi sasa baada ya kuachana nae mwishoni mwa msimu uliopita.


Simba ilitangaza hadharani kupitia kwa Msemaji wake kuwa inajiandaa kumuaga Kiungo wao aliedumu Klabuni hapo kwa miaka 13 kwa heshima kubwa katika tamasha lao la Simba Day.


Sasa utambulisho wa Mkude Yanga huenda unakwenda kufuta zoezi hilo lakini aliekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram aewapa Simba masharti ya kumuaga Mkude.


Manara ameandika


"Nimeona Somewhere, Afisa habari wa Madunduka akisema wamepanga kumuaga kwa Parade mchezaji wetu.


Yanga hatuna shida ya yeye kuja kuagwa siku ya Makolo Day, Tutashkuru mkimpa hiyo heshma Mchezaji wetu.


Ila inabidi muombe kwa maandishi na yasipungue maneno Elfu moja kwenye barua yenu ya maombi, na lazma hilo andiko liandikwe na Anko Mudi mwenyewe!!


Sharti la Pili aje kuagwa akiwa amevaa Jezi ya Yanga tena ile ya Njano,mkiweza hayo masharti atakuja kuagwa, na ieleweke atakuja huku akisindikizwa na Wananchi Elfu moja uwanjani Siku hiyo, wote wawe wametinga Jezi zetu.


Otherwise mchukueni huyo Nungu Nungu hapo juu, mumuage On Behalf of Him.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz