Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wachezaji wanne wa kigeni wanatarajia kuungana na kikosi cha Simba nchini Uturuki baada ya taratibu zao za vibali kukamilika
Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo, imebainisha kuwa wachezaji Che Fondoh Malone, Willy Essomba Onana na Jean Baleke wameondoka nchini leo ambapo watatua Uturuki hapo kesho
Aidha winga Aubin Kramo yeye ataungana wenzake mchana wa leo akitokea kwao Ivory Coast wakati kiungo Fabrice Ngoma anakamilisha vibali vyake kabla ya kuanza safari kuelekea Uturuki
Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema kiungo Clatous Chama sio miongoni mwa wachezaji waliosafiri suala lake likiwa bado linashughulikiwa na uongozi
Wachezaji wengine wanaendelea na mazoezi huko Uturuki leo ikiwa ni siku ya tano
No comments:
Post a Comment