Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amesema taratibu zote za ndani zimeshakamilika
"Leo ni siku ya mapumziko lakini si unaona tuko kazini?Tunaweka mambo sawa ili tuanze kutambulisha wachezaji wetu"
"Tumewasikia Wanachama wetu wanalalamika, wamechoka kusubiri, Rais ametuagiza tutambulishe wachezaji, tuko tayari"
"Tuliwaahidi baada ya kocha kuwasili tutawatangazia benchi la ufundi, zoezi ambalo tutalifanya wakati wowote"
"Kama tulivyosema tangu mapema, usajili wetu tulishaukamilisha muda mrefu, sasa wakati wa kuwafahamu wachezaji umefika," alisema Kamwe
Kulingana na taarifa ambayo iliyotolewa na Yanga mapema wiki hii, wachezaji wanapaswa kuripoti kambini Avic Town siku ya kesho Jumatatu, Julai 10
Ni takribani wiki nne zimebaki kabla ya msimu wa 2023/24 kuanza ambapo mechi za Ngao ya Jamii zitaanza August 09 Yanga ikichuana na Azam Fc
Post a Comment