Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa Yanga SC, wamefungiwa kusajili, Wananchi kupitia kwa Afisa Habari Ali Kamwe wamefunguka.
Taarifa ya Yanga kufungiwa usajili ilisambaa jana kwenye mitandao ya kijamii ambapo barua iliyosemekana ni ya kutoka FIFA, ilieleza kuwa Yanga wamefungiwa usajili tangu Juni 25, 2023 kwa kushindwa kumlipa aliyekuwa kocha wao, Luc Eymael.
Baada ya taarifa hiyo kusambaa kwa kasi na kuzua sintofamu, Ali Kamwe aliibuka na kueleza kuwa suala hilo halina ukweli wowote.
“Yanga Hatujafungiwa kusajili, wanatuzushia hizi habari ili kutuvuruga. Ni kweli tunadaiwa na Kocha lakini tunaendelea kumlipa kama tulivyotakiwa kufanya kisheria,” Ali Kamwe.
Post a Comment