Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kundi la mashabiki wa Manchester United wanapanga maandamano dhidi ya familia ya Glazers kwenye duka la vifaa vya michezo la klabu hiyo vile vya chapa ya Adidas.
Tukio hilo litafanyika leo asubuhi kwenye uzinduzi wa jezi mpya zitakazovaliwa msimu ujao.
Mashabiki hao wamechukizwa na familia ya Glazers kwa sababu mpaka sasa hawaelewi kama klabu itauzwa baada ya mchakato kudumu kwa muda miezi tisa au la.
Zikiwa zimebaki wiki saba msimu mpya uanze, bado haijafahamika nani aliyeshinda zabuni katika kinyang’anyiro kati ya mwekezaji kutoka Qatar, Jassim bin Hamad al-Thani na bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ractliffe.
Familia ya Glazers imetumia zaidi ya Pauni bilioni moja tangu ilipoinunua 2005 lakini mpaka sasa bado haijaamua licha ya ofa kuweka mezani na muda wake kupita.
Inaelezwa kwamba kundi la mashabiki limeamua kuandamana nje ya duka hilo lililopo katika Uwanja wa Old Trafford. Lengo la mashabiki hao wenye hasira inaelezwa ni kushinikiza wawekezaji hao wa sasa kuachia ngazi haraka iwezekanavyo kwani wamechoshwa.
Post a Comment