Vurugu uwanja wa Mkapa zaibuka bungeni Mapya Yaibuka - EDUSPORTSTZ

Latest

Vurugu uwanja wa Mkapa zaibuka bungeni Mapya Yaibuka

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Sakata la vurugu zilizosababisha kifo cha shabiki mmoja na wengine 29 kujeruhiwa siku ya pambano la fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger ya Algeria, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa limeibuka tena juzi bungeni, jijini Dodoma.


Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM), ndiye aliyeibua hoja hiyo kwa kuhoji ni kwanini serikali haiweki utaratibu mzuri wa kuingia uwanjani hadi kufikia mashabiki kukanyagana.


Katika mchezo huo wa kwanza wa fainali ulioisha kwa Yanga kufungwa mabao 2-1, shabiki wa timu hiyo, William Ernest alifariki kwa kukanyagwa baada ya kusukumwa kwanye geti la kuingilia uwanjani, huku majeruhi wengine wakilazwa kabla ya kuruhusiwa kwenye Hospitali ya Temeke.


Akichangia bungeni wakati wa majadiliano ya bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Chumi alisema kunatakiwa kuwekwa utaratibu mzuri wa kuingia uwanjani kwani mashabiki wamekuwa wakipata shida wakati wa kuingia uwanjani.


“Natoa pole kwa ile familia lakini lazima ifike wakati tujifunze wakati wa mechi kubwa jinsi ya kuingia uwanjani kwa usalama haiwezekani mechi inachezwa saa 10 jioni uende uwanjani asubuhi tuweke utaratibu mzuri,” alisema Chumi


Wakati akiendelea kuchangia alisimama Mbunge wa Mbinga Vijijini Benaya Kapinga (CCM) na kumpa taarifa Chumi kwamba uingiaji katika Uwanja wa Mkapa haupo vizuri. Mwenyekiti wa Bunge ambaye alikuwa akiongoza kikao hicho,Daniel Sillo ndiye aliyemruhusu Kapinga kumpa taarifa Chumi.


“Napenda kumpa taarifa uwanja wetu una mageti mengi lakini utaratibu uliozoeleka mageti yanayofungiliwa ni matatu tu lakini uwanja wote umezungukwa na mageti hali ambayo inasababisha watu wanasongamana,”alisema Kapinga.


Chumi alisema anapokea taarifa hiyo kwa sababu inaboresha namna ya kuingia uwanjani ambapo amedai kwenda uwanjani isiwe kero.


Pia, mbunge huyo alihoji ni kwanini mpaka sasa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) hakijafanya uchaguzi mpaka sasa.


“Niwaombe BMT jambo hili ni muhimu kama tunazungumzia kuinua soka la wanawake basi uchaguzi ufanyike,” alisema Chumi.


Chanzo: Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz