Simba yarejea kwenye misingi yake ya soka - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba yarejea kwenye misingi yake ya soka

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Simba inataka kurudisha mfumo wake wa kukuza vijana na kuwapa nafasi kwenye timu yao ya wakubwa ‘senior team’.

Leo imewatambulisha Selemani Matola kama Kocha Mkuu wa timu za vijana pamoja na Patrick Rweyemamu ambaye anakuwa Mkuu wa Prigram za soka la vijana.

Matola na Rweyemamu kwa pamoja wamewahi kuwa sehemu ya timu ya vijana ya Simba iliyowatoa nyota wengi kama Ibrahim Twaha, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Abdallah Seseme, Jonas Mkude n.k.

Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema, timu nyingi kubwa za Afrika zina timu imara za vijana ambao baadae wanaingia kwenye timu ya wakubwa.

Kwa upande wa Mkuu wa Program za vijana Patrick Rweyemamu yeye amesema, kuanzia mwaka 2008 hadi 2015 Simba kupitia timu ya vijana ilitoa wachezaji takriban 250. Akaongeza kuwa kuanzia madaraja ya chini kabisa hadi Ligi Kuu hakuna timu imewahi kukosa mchezaji aliyepita timu ya vijana ya Simba.

Selemani Matola ambaye ni Kocha Mkuu wa timu za vijana amsema Simba ilishawahi kufanikiwa katika soka la vijana, anaamini sasa hivi watazalisha wachezaji bora zaidi ya wale waliopita.

Ikumbukwe kuwa, Klabu ya Simba miaka ya nyuma ilikuwa ikikuza vipaji vya vijana wake kisha kuwapandisha daraja kwenda timu kubwa baada ya kuiva kikamilifu.

Miongoni mwa vijana hao ni Suleimani Matola, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, hamisi Ndemla, Musa Hassan Mgosi, Ally Salim, Miraj Adam, Abuu Hashimu, Ramadhani Kipalamoto, William Lucian ‘Gallas’, Hassan Hatibu, Ramadhani Singano ‘Messi’, Haroun Chanongo, Rashid Ismail, Edward Christopher, Hassan Isihaka na wengine.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz