Majaliwa: Tuiombee Yanga irejee na Kombe - EDUSPORTSTZ

Latest

Majaliwa: Tuiombee Yanga irejee na Kombe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuungana kwa pamoja kuiombea timu ya Yanga kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger utakaopigwa Juni 3, 2023 Algeria.

Akiwa bungeni Jijini Dodoma, Majaliwa amesema ni wakati wa Watanzania kuungana ili kuandika historia kwa pamoja na hana shaka na uwezo wa Yanga.

“Timu yetu ina uwezo mkubwa hivyo tuiombee, niungane na watanzania wenzangu kumshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa usafiri kwa Yanga, Mwenyezi Mungu awatangulie ili wakaandike historia” Amesema Waziri mkuu

Yanga wameondoka hapa nchini leo Juni 1 kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo huo ambapo wanahitaji ushindi wenye faida kwao ili kuwa mabingwa wa kombe la shirikisho Afrika.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz