Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba huenda ikamrejesha kocha wa magolikipa Milton Nienov ambaye amemaliza mkataba na Yanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amebainisha kuwa wamefanya tathmini ya mambo yaliyowakwamisha kushinda taji lolote msimu huu
Uongozi wa Simba umedhamiria kufanya marekebisho katika usajili wa wachezaji pamoja na maboresho ya benchi la ufundi
Nienov alijiunga na Yanga baada ya Simba kusitisha mkataba wake sambamba na Kocha viungo Adel Zrane na Didie Gomez aliyekuwa kocha mkuu
Simba ilichukua uamuzi huo mwaka 2021 baada ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na Jwaneng Galaxy
Aidha Simba pia inahusishwa na Kocha wa viungo kutoka klabu ya Rayon Sport Hategekimana Corneille
Corneille amewahi kufanya kazi na Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira wakati akiinoa Rayon msimu wa 2018/19
Post a Comment