Samatta: Kauli ya mimi kurudi SImba naomba muifute - EDUSPORTSTZ

Latest

Samatta: Kauli ya mimi kurudi SImba naomba muifute

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mshambuliaji na nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambaye pia ni mchezaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amewataka Watanzania wafute kauli yake ya kwamba ipo siku atarejea tena Simba SC.


Samatta ambaye aliwahi kuichezea Simba kabla ya kwenda TP Mazembe ya Congo DR, kisha KRC Genk, Aston Villa na baadaye Uturuki kisha akarudi tena Genk amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds FM.


Ikumbukwe kuwa, Samatta aliwahi kusema kuwa anatamani akistaafu soka la Kimataifa arejee Simba kama kocha kwani Simba ndiyo timu kubwa hapa nchini ambayo ilimtambulisha katika ulimwengu wa soka.


"Ni kweli nilishawahi kusema nitarudi Simba ila sasa naomba kauli hii tuifute kwanza, maisha yanabadilika you never Know wacha wakati ufike kwanza kisha tutajua," amesema Samatta.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz