Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa, mshambuliaji Fiston Mayele anarejea nchini kuungana na familia yake
Mengi yanazungumzwa kuhusu hatma yake na klabu ya Yanga lakini mwenyewe amesisitiza uongozi ndio unafahamu hatma yake
"Nimemaliza majukumu ya timu ya Taifa, sasa narejea Tanzania kuungana na familia yangu, mke na watoto wangu wanaishi Tanzania"
"Nimesikia huko Tanzania Thank You ndio neno linalotamba sana na kuna watu wanasubiri Thank You yangu, hilo sio jukumu langu, nimewaachia viongozi wa Yanga"
"Kwa sasa narejea kuungana na familia yangu kwa ajili ya mapumziko," alisema Mayele wakati akijibu maswali ya mashabiki kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Klabu ya Yanga imethibitisha kupokea ofa kadhaa za timu zinazomuhitaji Mayele ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Wananchi
Yanga imepanga kufanya nae mazungumzo ili kumuongeza mkataba na kama kutakuwa na ofa nono zaidi wanaweza kuridhia aondoke sasa ili wapate fedha kwani wakimuacha mpaka msimu ujao ataondoka akiwa mchezaji huru na Yanga haitapata chochote kutoka kwenye uhamisho wake
Post a Comment