Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi alijikuta akimwaga machozi mara tu baada ya mwamuzi wa mchezo wa Fainali kati ya Yanga dhidi ya USM Algiers.
Yanga ambao walionesha kiwango safi katika mchezo huo walijikuta wakiwa katika wakati mgumu kutokana na matukio mbalimbali yasiyo ya kiuanamichezo kutoka kwa Mashabiki wa USM Algiers.
Mbali na Nabi, Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele pia alijikuta akiangua kilio baada ya kulikosa Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga wamejikuta wakiukosa ubingwa na kwenda kwa USM Algiers waliokuwa na faida ya kufunga magoli mengi ugenini waliposhinda mabao 2-1 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0, lakini faida ya bao la ugenini ikawabeba USM Algiers.
No comments:
Post a Comment