Leo ni siku ya mwisho ya De Gea Man United

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mkataba wa Golikipa David De Gea na klabu yake ya Manchester United unamalizika leo June 30, 2023. Hivyo raia huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 32 atakuwa mchezaji huru kujiunga na timu yoyote itakapofika Julai 01, 2023.


Kwa miezi kadhaa golikipa huyo amekuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya lakini mpaka leo bado hawajafikia makubaliano ya mkataba mpya. Inaripotiwa kuwa The Red Devils walitaka De gea apunguze mshahara wake wa sasa wa pauni 275,000/= ili apewe mkataba mpya.


Inaelezwa kuwa Degea alikubali na alisaini mkataba huo lakini inadaiwa Manchester United wanataka apunguze mshahara wake zaidi, taarifa nyingine zinadai kuwa kocha Erik Ten Hag hamataki tena De gea na anampango wa kumsajili golikipa wa Inter Milan Adre Onana ambaye aliwahi kufanya nae kazi katika klabu ya Ajax.


David De gea ameitumikia Manchester United kwa misimu 12, alijiunga na kikosi hicho msimu wa 2011-12 akitokea Atletico Madrid ya Hispania. Ameichezea Man United jumla ya michezo 545 ameshinda makombe 8 akiwa na kikosi hicho. Ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England EPL mara 1, FA Cup, Europa League, Carabao Cup mara 2 na ngao ya jamii mara 3.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post