Kocha athibitisha Messi kuondoka PSG - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha athibitisha Messi kuondoka PSG

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kocha mkuu wa PSG, Christopher Galtier amethibitisha kuwa mshambuliaji Lionel Messi ataondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu baada ya kuhudumu ndani ya Mabingwa hao wapya wa Ligue1 kwa miaka miwili.


Akizungumza katika mkutani na waandishi wa habari Galtier (56) raia wa Ufaransa amethibitisha kuwa mchezo wa Jumamosi wa PSG dhidi ya Clermont Foot utakuwa mechi ya mwisho kwa Lionel Messi ndani ya uzi wa miamba hiyo ya Ufaransa.


Messi alijiunga na PSG baada ya mvutano wa kimaslahi na Barcelona mnamo 2021 na ameshinda mataji mawili ya Ligue 1, ingawa hajafanikiwa kutimiza lengo kuu ya PSG kumsajili la kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Kwa mujibu wa ripoti Muargentina huyo anaweza kurejea Barcelona lakini hali mbaya kiuchumi ya Mabingwa hao wa Laliga ndio kikwazo.


Inaelezwa kuwa Messi huenda akatimkia Marekani kunako klabu ya Inter Miami huku vilabu kadhaa vya Saudi Arabia vikimmezea mate.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz