Alicho kiandika Ahmedy Ally kuhusu tuzo zilizo tolewa na Tff jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kiandika Ahmedy Ally kuhusu tuzo zilizo tolewa na Tff jana

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Siku moja baada ya tuzo kwa waliofanya vizuri msimu wa 2022/23 kutolewa, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema washahitimisha rasmi msimu.


Kupitia Instagram Ahmed amewapongeza waliotwaa ubingwa na waliopata tuzo na wasimamizi wa Ligi pamoja na waaandaji wa tuzo.


"Kwetu Simba tuwapongeze nyota wetu waliotwaa tuzo hakika wametuheshimisha. Kiujumla kama timu hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji msimu huu," ameandika Ahmed na kuongeza


"Hii inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa msimu ujao. Ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imara. Ni jukumu letu viongozi kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti, na hilo limeshaanza kufanyika kwa umaridadi wa hali ya juu sana," ameandika Ahmed


Meneja huyo ameeleza kiu na shauku kubwa ya Wanasimba ni kuona mataji yanarejea kwenye timu yao kwani wamechoka kelele za jirani


"Timu kubwa kama Simba haipaswi kukaa muda mrefu bila mataji, miaka miwili inatosha ni muda sasa wa kurudisha ufalme na wetu. Tukutane 2023/2024,"


Chanzo: MwanaspotiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz