Yanga watua Dar, fasta waunganisha safari Singida - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga watua Dar, fasta waunganisha safari Singida

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kikosi cha Yanga kimewasili salama Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam kikitokea Afrika Kusini ambako juzi kilikata tiketi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwatoa wenyeji, Marumo Gallants.


Na baada ya kuwasili Yanga wanaunganisha safari kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars Jumapili.


Yanga imeitoa Marumo Gallants ya kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini Jumatano na kwenye Fainali itakutana na USM Alger ya Algeria.


Yenyewe USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.


Yanga itaanzia nyumbani katika Fainali ya kwanza Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria kwa mchezo wa marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.


Tayari Yanga wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo wakiwa wana mechi mbili mkononi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz