Yanga waiandikia bodi ya ligi barua kuomba jambo hili - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga waiandikia bodi ya ligi barua kuomba jambo hili

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wameiandikia barua Bodi ya Ligi Kuu kuomba 'review' ya Ratiba kutokana na mfululizo wa mechi zinazowakabili


Jana Yanga ilikwama kutua Dodoma wakati ikiwa safarini kuelekea Singida na kulazimika kurejea jijini Dar es salaam kutokana na changamoto ya taa kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma


Injinia Hersi amesema wanafanya utaratibu kuhakikisha timu inasafiri mkoani Singida haraka iwezekanavyo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars ambao utapigwa Alhamisi, May 04 katika uwanja wa Liti


"Tunawasiliana na Mamlaka za soka nchini, tumewaomba wafanye review ya ratiba ya mechi zetu kwani sio rafiki kwa afya za wachezaji"


"Tunapaswa kucheza na Singida BS mechi ya ligi kuu May 04 halafu kucheza nao tena mechi ya nusu fainali kombe la FA May 07"


"Tunakabiliwa na mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la CAF May 10, tunapaswa kusafiri kutoka Singida kurejea Dar baada ya mchezo dhidi ya Singida BS May 07"


"Hakuna usafiri wa ndege kutoka Singida kuja Dar maana yake ni kuwa tutalazimika kusafiri kwa njia ya basi mpaka Dodoma na tutafika Dar May 08 kwa hiyo tutakuwa na siku moja tu ya kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya CAF"


"Wanasema mcheza kwao hutuzwa, tukiwa wawakilishi wa nchi tumeomba tupewe muda wa kujiandaa na mchezo dhidi ya Malumo Galants," alisema Hersi



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz