Mfahamu Youssouph Dabo kocha mpya wa Azam FC - EDUSPORTSTZ

Latest

Mfahamu Youssouph Dabo kocha mpya wa Azam FC

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Jina lake kamili ni Youssouph Dabo. Alizaliwa Novemba 11, 1979 mjini Sagatta nchini Senegal. Kwa sasa ana miaka 43 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Azam FC kuanzia msimu ujao 2023/24.


Alicheza soka nchini mwake kisha Tunisia na baadaye Ufaransa ambako alicheza madaraja ya chini. Alipostaafu akasomea ukocha na akaanza rasmi mwaka 2012. 


Mafanikio yake kama kocha. Mwaka 2016, akiwa na Tengueth alishinda ubingwa wa Kombe la Ligi. 


Mwaka 2017 akiwa kocha wa Tengueth alifika fainali ya Kombe la Senegal (sawa na Kombe la Shirikisho la Azam hapa nchini) 


Desemba, 2018 alitwaa ubingwa wa vijana chini ya miaka 20 kwa timu za taifa ukanda B wa Afrika Magharibi (mashindano yalipofanyika Togo). 


Februari 2019 alichaguliwa kuwa kocha bora wa Afcon chini ya miaka 20 huko Niger alipoisaidia Senegal kufika fainali. 


Juni 2019 aliiongoza Senegal kufika robo fainali ya Kombe la Dunia chini ya miaka 20 nchini Poland.


Julai 2019 alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Senegal iliyofika fainali ya Afcon kule Misri. 


Agosti 2019 akiwa kocha wa timu ya taifa ya Senegal chini ya miaka 23, aliiongoza kushika nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba kwenye michezo ya Afrika jijini Rabat, Morocco.


Desemba 2019 aliiongoza Senegal kushinda ubingwa wa kanda ya Wafu mashindano yaliyofanyika Guinea. 


Machi 2020 aliiongoza Senegal kushinda ubingwa vijana chini ya miaka 20 wa mashindano ya mataifa ya Kiarabu. Senegal ilishiriki kama wageni waalikwa mashindano yaliyofanyika Saudi Arabia. 


Novemba 2020 akiwa kocha wa timu ya taifa ya Senegal chini ya miaka 20 walifika fainali kuwania ubingwa wa kanda A ya Afrika Magharibi. 


Msimu wa 2020/21 alishinda ubingwa wa ligi ya Senegal akiwa na Tengueth.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz