Watumishi saba wasimamishwa kazi kukatika kwa umeme Uwanja wa Mkapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Watumishi saba wasimamishwa kazi kukatika kwa umeme Uwanja wa Mkapa

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Serikali imewasimamisha kazi watumishi saba akiwemo Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Salum Mtumbuka kufuatia hitilafu ya kuzimika kwa taa katika uwanja huo iliyojirudia wakati Yanga ikicheza dhidi ya Rivers United kutoka Nigeria.


Mwezi Machi mwaka huu taa hizo zilizimika wakati Taifa Stars ilipowakaribisha Ugandan Cranes ya Uganda katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). 


Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema Waziri Pindi Chana amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuchukua hatua. 


“Katibu Mkuu Saidi Yakubu amewasimamisha kazi watumishi wanaohusika na uendeshaji wa uwanja kupisha uchunguzi,” imesema taarifa ya Wizara.


Waliosimamishwa ni Manyori Juma Kapesa (Mhandisi wa Umeme wa Uwanja), Tuswege Nikupala (Afisa Utawala wa Uwanja), Dk. Christina Luambano, Yanuaria Imboru, Gabriel Mwasele na Gordon Nsajigwa Mwangamilo. 


Katibu Mkuu Yakubu amemteua Milinde Mahona kukaimu nafasi ya Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia leo Mei Mosi, 2023.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz