Wasauzi wamuwinda Fei Toto - EDUSPORTSTZ

Latest

Wasauzi wamuwinda Fei Toto

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wakati kamati ya hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) likisisitiza kuwa Feisal Salum "Feitoto" ni mali ya Yanga SC, klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini (PSL) Sekhukhune United imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo huyo wa timu ya taifa ya Tanzania.


Inasemekana mazungumzo kati ya klabu hiyo pamoja na wawakilishi wa Feisal Salum yameanza na klabu hiyo inamhitaji kiungo huyo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo.


Sekhukhune United waliomaliza wakiwa nafasi ya saba(7) kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Afrika Kusini wanatumia uwanja wa Peter Mokaba Stadium uliopo kwenye jiji la Polokwane.


Hawa wameanza maboresho ya kikosi chao kuelekea msimu ujao na tayari wameanza mazungumzo na wawakilishi wa Feisal Salum "Feitoto".Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz