Gundu! Mane na mastaa wenzake waliofulia baada kumkimbia Klopp - EDUSPORTSTZ

Latest

Gundu! Mane na mastaa wenzake waliofulia baada kumkimbia Klopp

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Jurgen Klopp ni bonge la kocha na hilo halina mjadala. Kile ambacho amefanya Mainz 05, Borussia Dortmund na sasa Liverpool kimejionyesha bayana.


Chini yake wamepita mastaa kibao. Na chini yake amewapiga bei mastaa wa maana kabisa kwenye mchezo wa soka. Lakini, unaambiwa hivi, usithubutu kumlazimisha Klopp akupige bei, itakwenda kula kwako huko unakoenda.


Kuthibitisha hilo cheki hapa kilichowatokea mastaa ambao walilazimisha kuuzwa na kocha Klopp kile kilichokwenda kuwatoa huko walikokwenda baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa cha soka walipokuwa chini yake.


SADIO MANE


Presha ilikuwa kubwa Liverpool juu ya mikataba mipya ya mastaa wawili kwenye safu ya ushambuliaji, Sadio Mane na Mohamed Salah. Mane alikuwa anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Anfield na Liverpool hawakutaka kumuuza, lakini walilazimika kukubali ofa ya Pauni 27 milioni tu ili asiondoke bure kumruhusu Mane aende Bayern Munich baada ya kulazimisha kuondoka. Lakini, tangu alipofika Allianz Arena mambo yamekuwa tofauti kabisa kwa Mane, hana maajabu na kocha Thomas Tuchel ameripotiwa kwamba hahitaji kumwona akiendelea kukipiga kwenye kikosi chake msimu ujao.


MARIO GOTZE


Gotze alikuwa moto sana huko Borussia Dortmund chini ya Klopp, lakini staa huyo alilazimisha kuondoka kwenda Bayern Munich kwa ada ya Pauni 35 milioni kwenye msimu wa 2012-13. Tena Dortmund ilikosa huduma ya Gotze kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich kwa madai kwamba mchezaji huyo alikuwa majeruhi na msimu ulipokwisha alikwenda kujiunga Allianz Arena. Alifunga bao kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka mmoja baada ya uhamisho wake, lakini Gotze hakuwa na wakati mzuri Bayern kwa kulingananisha na ubora wake wa Dortmund.


PHILIPPE COUTINHO


Moja ya mauzo ya kibabe kabisa aliyowahi kufanya Klopp ni wakati alipomuuza Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa ada ya Pauni 140 milioni. Wakati Mbrazili huyo alikuwa staa wa maana kabisa Liverpool na kucheza soka la kibabe, lakini kila kitu kilikuwa tofauti baada ya kwenda kutua Barcelona, ambako aliishia tu kutolewa kwa mkopo kabla ya kuuzwa jumla huko Aston Villa. Klopp yeye alitumia pesa aliyomuuza Coutinho kuwasajili Virgil Van Dijk na Alisson, ambao wamekuja kumpa taji la kwanza la Ligi Kuu England. Bila shaka Coutinho alijita kuondoka Liverpool.


GEORGINIO WIJNALDUM


Ilishangaza sana kuona kiungo wa Kidachi Georginio Wijnaldum kuchagua kuachana na mpango wa kusaini dili jipya Liverpool na ilionekana kabisa anakwenda kujiunga na Barcelona mwaka 2021. Lakini, dakika za mwisho kabisa staa huyo alikwenda kujiunga na PSG baada ya kupewa ofa ya kulipwa mara mbili ya mshahara wake. PSG inapenda kusajili mastaa wenye majina makubwa, lakini uhamisho wa Wijnaldum huko Parc des Princes haikuwa mzuri kabisa, staa huyo hakuwa kwenye ubora wake. Wijnaldum alikuwa kwenye kiwango bora sana chini ya Klopp huko Liverpool, lakini alipoondoka mambo yakatibuka.


XHERDAN SHAQIRI


Winga wa Uswisi, Shaqiri alipita Bayern Munich na Inter Milan kabla ya kutua Stoke City, ambako alionwa na Liverpool na kunaswa mwaka 2018. Klopp alikuwa akimtumia kama super-sub na hakika Shaqiri alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Liverpool kutokana na soka matata alilokuwa akicheza, lakini baada ya kujiuga na Lyon mwaka 2021 mambo yamekuwa magumu akihangaika kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Mambo yalizidi kuwa magumu Ligue 1, hivyo akatimkia zake Chicago Fire ya Marekani baada ya kucheza kwenye soka la Ufaransa kwa miezi sita tu. Shaqiri wa Liverpool alikuwa noma.


SHINJI KAGAWA


Kiungo mchezeshaji wa Kijapani, Shinji Kagawa alikuwa moto kwelikweli Borussia Dortmund na hilo liliwafanya Manchester United kutoa mkwanja mwaka 2012 kunasa saini yake wakati huo wakiwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson. Chini ya Klopp, Kagawa alikuwa maarufu sana, lakini maisha yake huko Old Trafford hayakwenda kuwa matamu na matokeo yake alidumu kwa misimu miwili tu kabla ya kurudi Dortmund. Kama ilivyotokea kwa Gotze, Kagawa naye awamu yake ya pili Dortmund haikuwayenye kuvutia kabisa, lakini alichoambulia Man United ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England.


NURI SAHIN


Nuri Sahin alikuwa mzuri sana alipokuwa Borussia Dortmund na alikuwa akisakwa na kila timu ya Ulaya kabla ya kuachana na timu ya Klopp kwenda kujiunga Real Madrid mwaka 2011. Yalikuwa makosa makubwa. Matokeo yake, kiungo huyo wa Kituruki, alikwenda kucheza mechi 10 tu Real Madrid kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Liverpool. Kama ilivyokuwa kwa mastaa wengine kwenye orodha hii, Sahin alirejea Dortmund, lakini hakuwa tena kwenye ubora ule kama alivyokuwa awali. Sahin anaingia kwenye orodha ya wakali wa maana sana waliocheza soka la kibabe chini ya Klopp kabla mambo kutibuka alipouzwa.


EMRE CAN


Staa wa kimataifa wa Ujerumani, Emre Can alikuwa mchezaji wa uhakika na muhimu kwenye kikosi cha Liverpool chini ya kocha Klopp, lakini aligoma kusaini mkataba mpya na kwenda kutimkia bure Juventus wakati mkataba wake huko Anfield ulipofika tamati 2018.


Can alidhani kwamba kwa kuhamia Juventus anakwenda kukuza soka lake, lakini badala yake ni kama alipishana na mambo mazuri, kwani Liverpool ilikwenda kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku yeye akiwa na nyakati ngumu Turin. Can mambo yalitibuka hadi aliondolewa kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019.


Chanzo: MwanaspotiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz