USAJILI: Yanga yajitosa kumsajili Chivaviro - EDUSPORTSTZ

Latest

USAJILI: Yanga yajitosa kumsajili Chivaviro

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Habari kubwa iliyotamba kwenye mitandao ya kijamii jana ni kuhusiana na mshambuliaji wa Marumo Gallants Ranga Chivaviro ambaye anahusishwa na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga Sc


Chivaviro anatarajiwa kuachana na Marumo mwishoni mwa msimu baada ya timu hiyo kushuka daraja kipaumbele chake kikiwa kujiunga na timu ambayo itashiriki michuano ya CAF msimu ujao


Katika moja ya mahojiano na vyombo vya Habari Afrika Kusini, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliahidi kuwa Yanga itasajili mshambuliaji mmoja kutoka ligi kuu ya Afrika Kusini


Khanyisa Mayo wa Cape Town City na Ranga Chivaviro ndio wachezaji waliokuwa wakilengwa na Injinia Hersi


Jana Wakala wa Chivaviro akathibitisha kuwepo kwa mazungumzo kati yao na Yanga huku akieleza kuwa Chivaviro amevutiwa zaidi na ofa iliyotolewa na Yanga licha ya Azam Fc nayo kumuhitaji


Chivaviro ni mmoja wa washambuliaji waliofanya vizuri katika ligi kuu ya Afrika Kusini msimu huu licha ya timu yake ya Marumo Gallants kushuka daraja


Amefunga jumla ya mabao 16, akifunga mabao 10 kwenye ligi na mabao sita kwenye kombe la Shirikisho sawa na Fiston Mayele wa Yanga


Mayo na Peter Shalulile ndio vinara wa mabao ligi kuu ya Afrika Kusini kila mmoja akifunga mabao 12


Ikiwa imetinga fainali ya kombe la Shirikisho msimu huu, Yanga inajipanga kuhakikisha msimu ujao inafanya vyema katika michuano ya Ligi ya MabingwaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz