Simba iko kamili kuivaa Azam fc kesho, Mgunda, Zimbwe wafunguka

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Simba iko tayari kwa mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili, May 07 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara


Kocha Msaidizi wa Simba Juma Mgunda amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri kuelekea mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa mgumu


"Maandalizi ya mchezo yamekamilika, wachezajii wote wako kwenye hali nzuri. Tunajua utakuwa mchezo mgumu, tunawaheshimu Azam Fc kwa kuwa ni timu nzuri"


"Hata hivyo sisi tumejipanga tukihitaji kushinda ili tuweze kuingia fainali ya michuano hii," alisema Mgunda


Akizungumzia maandalizi ya mchezo, Mgunda amesema watakuwa na mabadiliko ya kimbinu kwa sababu utakuwa mchezo wa mtoano ambao lazima mshindi apatikane


Amesema Azam Fc walipata matokeo mazuri dhidi ya Simba kwenye ligi hivyo watahitaji kuwa bora kimbinu ili kuhakikisha wanapata ushindi


"Katika mechi za ligi msimu huu wamefanya vizuri dhidi yetu lakini mchezo wa kesho ni tofauti na mtoano kwahiyo hata mbinu zitakuwa tofauti, tumejipanga kwa ajili ya kupata ushindi"


Nae nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema matumaini ya Simba kushinda taji msimu huu yamebaki katika kombe la FA hivyo watapambana kuhakikisha wanapata ushindi


"Matumaini yetu yamebaki zaidi kwenye michuano hii, tunajua ugumu na umuhimu wa mchezo lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunapata ushindi," alisema

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post