Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya ushindi dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini uliowahakikishia kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, leo Yanga inawania fainali nyingine katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS ambao utapigwa saa 9:30 alasiri
Kikosi cha Yanga kiliwasili mkoani Singida mapema jana na jioni kufanya mazoezi ya mwisho katia uwanja wa LITI
Huu ni mchezo wa pili kuzikutanisha Yanga na Singida BS katika uwanja wa Liti msimu huu
May 05 timu hizo zilichuana katika mchezo wa ligi kuu na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Kocha Mkuu wa Singida BS Hans van Pluijm amesema wamefanya maandalizi mazuri na leo hawatarudia makosa waliyofanya katika mchezo wa uliopita kwenye ligi
Hata hivyo watalazimika kuwa katika ubora hasa kuweza kupata ushindi mbele ya Yanga ambayo wachezaji wake wana morali kubwa
Jambo pekee ambalo linaweza kuiathiri Yanga ni uchovu ambapo mabingwa hao wa Tanzania Bara wamefanya mazoezi mara moja tu tangu watoke Afrika Kusini
Baada ya ushindi dhidi ya Marumo May 17, Yanga iliondoka Afrika Kusini jioni ya May 18 na kuwasili jijini Dar es salaam Alfajiri ya May 19 ambapo siku hiyo jioni wakaunganisha kuelekea mkoani Dodoma ambako timu ililala
Jana May 20 asubuhi Wananchi wakaelekea mkoani Singida na jioni wakafanya mazoezi yao ya kwanza tangu walipochuana na Marumo
Hata hivyo Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema watakuwa na mabadiliko ya kikosi katika mchezo huo na wanafurahi kuwa na kikosi kipana wachezaji wote wako tayari
Mtanange huo utakuwa na dakika 30 za nyongeza kama hakutapatikana mshindi kwenye dakika 90 na baadae kupigwa mikwaju ya penati kama mchezo utamalizika kwa sare
Post a Comment