Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Imani Kajula amekiri kuwa ni kweli wachezaji wao hawajalipwa posho takribani Tsh milioni 20 lakini hiyo si sababu ya wao kushindwa kujituma na kuipa matokeo mazuri timu yao.
Kajula amesema hayo baada ya Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally kunukuliwa akisema kuwa wachezaji hao wanadai posho zao za michezo kadhaa ya nyuma.
Ikumbukwe kuwa, haya yote yameibuka baada ya Simba kuondolewa katika mbio za kuwania ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam, kuondolewa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika hatua ya robo fainali huku wakipoteza matumaini ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
"Timu yetu imeshatoa bonus zaidi ya Tsh bilioni 1.1 na kiasi kilichobaki ni sh milioni 20 pekee tena ni bonus ya Ligi ya ndani.
"Wewe vuta picha Klabu inalipa zaidi ya Sh bilioni illion 1.1, inashindwaje kulipa sh milioni 20? Haingii akilini hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu.
"Vuta picha wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya 30 kila mmoja atapata kiasi gani, ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi,” Imani Kajula Mtendaji Mkuu Simba SC.
Pia Mtendaji Mkuu Iman Kajula, amesema kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema itawalipa bonus ila huwa wanatoa kwa ajili ya kuwahamasisha wapandane zaidi kwenye kile wanachokipambania.
Post a Comment