'Mkwanja' wa Super League waiongezea jeuri Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

'Mkwanja' wa Super League waiongezea jeuri Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Uongozi wa klabu ya Simba umesema una uwezo wa kufanya usajili wa mchezaji yeyote wanayemtaka kwa ajili ya kuimarisha kikosi kwa kuwa fedha za kufanya hivyo wanazo


Simba inatarajia kupata fedha zaidi ya Sh. bilioni tano kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) za maandalizi ya michuano ya Super League lakini kuna fedha watakazozipata kutokana na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kiasi cha Dola za Marekani 900,000 (zaidi ya Sh. bilioni 2.1).


Simba inatarajiwa kutumia sehemu kubwa ya fedha hizo kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema wanaendesha mchakato wao wa usajili kwa umakini mkubwa.


"Bado hatujaweka wazi wachezaji tunaowataka ingawa yapo majina ya wachezaji tunaowataka, uongozi upo makini kufanya usajili wa nguvu kwa sababu fedha zipo"


"Tuna mzigo mkubwa ukiunganisha fedha za Wadhamini na mwekezaji wetu, Mohammed Dewji, fedha za Super League na vyanzo vingine, hii itatufanya kuwa na jeuri ya kufanya usajili kwa wachezaji tunaowataka," alisema AhmedDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz