Mamlaka zafuta kadi nyekundu ya Vinicius Jr - EDUSPORTSTZ

Latest

Mamlaka zafuta kadi nyekundu ya Vinicius Jr

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kamati ya mashindano ya Chama cha soka Nchini Uhispania (RFEF) imetoa maamuzi juu ya sakata la winga wa Real Madrid, Vini Jr ambapo imefuta kadi nyekundu aliyopewa Mbrazil huyo kwenye mchezo wa kipigo cha 1-0 cha Real Madrid dhidi ya Valencia.


RFEF imefikia uamuzi huo kwa kuwa adhabu hiyo ilitolewa chini ya ushahidi batili. Mwamuzi wa VAR hakumwekea Mwamuzi wa Kati picha zote zinazohusu matukio yaliyopelekea adhabu hiyo kutolewa.


Aidha Kamati hiyo imethibitisha kuwa klabu ya Valencia imetozwa faini ya Euro 45,000 pamoja na kuufungia kwa mechi 5 upande wa uwanja wa Mestalla uitwao Mario Kempes kusini, ambapo vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa Vini Jr vilitokea.


Vinicius Jr atakuwa huru kuitumikia klabu yake hiyo leo Real Madrid itakapomenyana na Rayo Vallecano majira ya saa 2:30 usiku katika dimba la Santiago Bernabeu.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz