Mayele afurahia msimu wa mafanikio akiwa na Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Mayele afurahia msimu wa mafanikio akiwa na Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema anajivunia kuhusika kwenye mafanikio ya timu yake ya Yanga katika michuano mbalimbali, huku akikiri kuwa huu ndio msimu bora zaidi kwake katika maisha yake ya soka


Akizungumza baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Singida Big Stars na Yanga uliopigwa jana mkoani Singida na yeye kufunga bao pekee katika mchezo huo, hivyo kuipeleka Yanga hatua ya fainali, amesema msimu huu umekuwa wa mafanikio kwake katika michuano ya kitaifa na kimataifa


"Nmeshiriki michuano ya CAF mara nyingi lakini sikuwahi kufunga mabao saba au sita, nilikuwa ninafunga, lakini mabao matatu au mawili kwa hiyo nina furaha sana na msimu huu," alisema Mayele


Mayele anaongoza katika ufungaji Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 16, lakini pia ana mabao sita katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga imeingia hatua ya fainali


Katika msimu huu Mayele amfunga mabao 33 katika mashindano yoteDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz