Manji arejea Yanga, amuulizia nahodha - EDUSPORTSTZ

Latest

Manji arejea Yanga, amuulizia nahodha

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Athuman Idd 'Chuji' amesema Mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Yusuf Manji alimuuliza alipo nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro'.


Manji aliibuka kwenye mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers juzi na kuzua gumzo kwa mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wamejazana kwenye mchezo huo, huku akipata bahati ya kukaa karibu na Chuji ambaye alifanya vizuri kipindi cha nyuma.


Huyu ndiye mfadhili wa mwisho wa timu hiyo, akiwa anatajwa kuwa mmoja kati ya watu waliopata mafanikio makubwa kwenye timu hiyo ya Twiga na Jangwani. Akisimulia jinsi ambavyo alikutana na Manji, Chuji alisema


"Nilishangaa nilipokuwa nimekaa nimeshikwa na mkono kwenye bega, nikaitwa Chuji ni wewe (Chuji it's you ), kugeuka nikamuona Manji, nikajikuta natawaliwa na ukimya wa furaha, nilikuwa sijui nifanye nini kwa wakati huo, ingwa na mimi nikamuuliza mwenyekiti ni wewe, akatabasamu tu na kuonyesha kufurahia uwepo wangu pale.


"Hata yeye alikaa kimya kwanza baada ya kuniuliza ni mimi, kisha tukakumbatia kwa furaha, akaniambia nimefurahi kukuta hapa sikutegemea, kwasababu nakutafuta kwa kipindi kirefu kijana wangu.


Stori za hapa na pale zikaendelea baina ya Chuji na Manji, wakikumbushiana nyakati wanafanya kazi Yanga na namna mechi ilivyokuwa inaendelea dhidi ya Rivers United.


Mbali na hilo, Chuji alisema mchezaji mwingine aliyeuliziwa na Manji ni Nadir Haroub 'Cannavaro' nahodha wa zamani wa timu hiyo.


"Aliniuliza Cannavaro yupo wapi nikamjibu yupo majuu (Marekani), akaniambia kwa nyakati zenu mlifanya kazi kwa bidii, hivyo mnaheshimika sana nafikiri bado ninyi ni watu muhimu sana," alisema.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz