Man Utd yaitega SSC Napoli kwa Kim Min-Jae - EDUSPORTSTZ

Latest

Man Utd yaitega SSC Napoli kwa Kim Min-Jae

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Manchester United imeripotiwa kuwapa Mabingwa wa Soka nchini Italia SSC Napoli Pauni Milioni 13 zaidi kwenye ofa yao ya kumsajili Kim Min-Jae kuliko bei anayouzwa mkali huyo wa kutoka Bara la Ásia.


SSC Napoli imekuwa ya moto msimu huu na kutwaa ubingwa wa Serie A huku ikiwa na mechi tano mkononi. Na kwenye kikosi chao kuna mchezaji Kim, ambaye huduma yake ya uwanjani imemkosha Meneja wa Man United, Erik ten Hag na anamtaka wakafanye kazi pamoja Old Trafford.


Kwa mujibu wa Corriere dello Sport, beki Kim, 26, kwenye mkataba wake imetajwa bei anayouzwa ni Pauni 40 milioni kama kutakuwa na timu ya kutoka nje ya Italia itahitaji saini yake kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.


Lakini, Man United kuonyesha wanahitaji sana huduma ya mkali huyo wa Korea Kusini, wapo tayari kulipa Pauni 53 milioni, ikiwa ni Pauni 13 milioni zaidi ya bei yake iliyopangwa.


Man United wanaamini jambo hilo litawashawishi SSC Napoli kufanya biashara kuliko kuwafikiria kama wapinzani hivi.


Man United inahitaji kuongeza beki mwingine kwenye kikosi chao ili isiwe shida kama Lisandro Martinez na Raphael Varane watakuwa majeruhi kama ilivyo kwa sasa na kulazimika kumchezesha beki wa kushoto Luke Shaw kwenye beki ya kati.


Beki Harry Maguire anatarajia kufunguliwa mlango wa kutokea mwisho wa msimu, huku huduma ya Kim ikiwa matata, akicheza mechi 33 huko SSC Napoli msimu huu na kufunga mara mbili.


SSC Napoli imecheza mechi 17 bila ya kuruhusu bao, huku timu hiyo ikifungwa mara 23 tu kwa shughuli ya Kim, ambaye alisajili kutoka Fenerbache mwaka jana.


Chanzo: Dar24Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz