Hawa hapa wachezaji wa Yanga watakao ukosa mchezo wa kesho dhidi ya Singida Bs - EDUSPORTSTZ

Latest

Hawa hapa wachezaji wa Yanga watakao ukosa mchezo wa kesho dhidi ya Singida Bs

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wachezaji Djigui Diarra na Khalid Aucho wataukosa mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa LITI kutokana na sababu mbalimbali


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabri mapema leo, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Diarra alipata matatizo ya kifamilia wakati Aucho aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Marumo Gallants


"Wachezaji wako tayari isipokuwa mpaka sasa tuna uhakika wa kuwakosa Djigui Diarra na Khalid Aucho ambao wana changamoto ambazo ziko nje ya uwezo wetu"


"Tumekuwa na muda mfupi tangu mchezo uliopita dhidi ya Marumo Gallants, zaidi tumefanya recovery kuondoa uchovu na leo tutakamilisha mazoezi ya mwisho"


"Kiakili tuko vizuri, tunaheshimu mpinzani ambaye tutacheza nae tunataka kushinda ili tuingie fainali," alisema Kaze


Winga Denis Nkane amesema pamoja na kukosa muda wa kufanya mazoezi, wachezaji wako tayari na wanatambua umuhimu wa mchezo huo wakihitaji kushinda waweze kutinga fainali



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz