Fei Toto aomba msaada acahngiwe pesa za kwenda CAS - EDUSPORTSTZ

Latest

Fei Toto aomba msaada acahngiwe pesa za kwenda CAS

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga, Mchezaji huyu leo ametangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS).


Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake; “Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heroes.


“Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS.


"Nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya Wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, heshima na haki zao naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya Kulipia gharama za kufungua Jalada la kesi yangu CAS ili kupata Haki yangu ya Kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba.


“Tafadhali naomba unichangie ili nipate haki yangu itakayoniwezesha kutumikia kipaji changu na Timu za Taifa (Tanzania na Zanzibar) katika namna tofauti kwa manufaa yangu na Taifa.


"Shangazi Fatma Karume na wanasheria wengine watafanya kazi bure, unaweza kulipia kwa lipa namba (5406394 FEISAL SALUM) hapo pichani au kwa namba hii ya simu kwa 0679 12 88 99 FEISAL SALUM ABDALLAH. NAOMBA UNICHANGIE," ameandika Feitoto.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz