Breaking: Yanga yatwaa ubingwa wa ligi kuu NBC 2022/2023 - EDUSPORTSTZ

Latest

Breaking: Yanga yatwaa ubingwa wa ligi kuu NBC 2022/2023

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuichapa Dodoma Jiji mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Kennedy Musonda aliitanguliza Yanga kabla ya Dodoma Jiji kufunga mabao mawili kupitia kwa Collins Opare na Seif Karihe

Ilikuwa presha kuwa kwa Yanga baada ya kuwa nyuma kwa muda mwingi wa kipindi cha pili lakini wakatumia dakika 15 za mwisho kuonyesha kwa nini wametwaa ubingwa msimu huu

Mudathir Yahya aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Stephane Aziz Ki alikuwa shujaa wa Wananchi leo akifunga mabao mawili

Aliisawazishia Yanga bao la pili kabla ya Farid Mussa kufunga la tatu na Mudathir kuongeza la nne kwenye dakika za majeruhi

Alama 74 zimeihakikishia Yanga kutwaa ubingwa ikiwa na michezo miwili mkononi kwani Simba hata ikishinda mechi zilizosalia itafikisha alama 73



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz