Zimbwe Jr, Robertinho wafunguka kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Zimbwe Jr, Robertinho wafunguka kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Yanga

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Oliveira amesema yeye anapendelea mechi za derby kwa sababu ni mchezo ambao wachezaji, makocha na hata mashabiki wanaupenda


"Tumefanya maandalizi mazuri, wachezaji wako tayari, hii ni mechi kubwa. Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tumejiandaa vyema kusaka ushindi"


"Nawaambia mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa, uwingi wa mashabiki utatupa nafasi ya kuwa na mchezaji wa 12 uwanjani," alisema Oliveira


Kwa upande wa kikosi, Robertinho amesema wachezaji wake wote wako tayari kwa mchezo huo


Nae nahodha msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema mchezo dhidi ya Yanga kesho ni kama fainali kwao kwani wanazihitaji alama zote tatu


Zimbwe Jr amesema wanahitaji ushindi ili kurejesha matumaini katika mbio za ubingwa


"Hii ni mechi kubwa, kwa utamaduni wa Simba na Yanga sio jambo zuri sisi kupoteza mchezo na kuwaruhusu watangaze ubingwa mbele yetu, hivyo hilo linatuhamasisha kuhakikisha tunapambana kwa jasho na damu ili kupata alama tatu"


"Lakini jambo muhimu zaidi kwetu hatutafuti ushindi ili kuizuia Yanga kutwaa ubingwa mbele yetu, bali hata sisi tuko kwenye mbio za ubingwa. Kama hatutapata ushindi tutapunguza nafasi yetu lakini ushindi utatuongezea nafasi kwani tutapunguza gap la pointi"


"Muhimu tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani , tunawaahidi watapata burudani na tumejipanga kushinda," alisema Zimbwe Jr



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz