Hawa hapa wachezaji wa Yanga watakao ikosa mechi ya kesho dhidi ya Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Hawa hapa wachezaji wa Yanga watakao ikosa mechi ya kesho dhidi ya Simba

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanatambua ugumu wa mchezo dhidi ya watani zao Simba lakini wamejiandaa vizuri na tayari kwa mchezo huo


Kaze amesema Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili, ni mchezzaji mmoja tu, Aboutwalib Mshery ambaye ni majeruhi


"Tumejiandaa vizuri kwa mchezo huu mkubwa. Tunafurahi tunakwenda kwenye mchezo tukiwa na wachezaji wote isipokuwa mlinda lango Aboutwalib Mshery ambaye yuko anaendelea na matibabu"


"Hii ni mechi kubwa lengo letu ni kushinda. Wakati wa maandalizi tumefanya kila kitu muhimu kwa ajili ya mechi yenyewe kitu kikubwa ni kuwa na kiwango bora, tuweze kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri"


"Umuhimu wa ushindi katika mchezo huu utatuweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, hivyo hii ni motivation kubwa kwa wachezaji wetu," alisema Kaze


Kaze pia amesema kucheza na Simba kabla ya mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ni kitu kizuri kwao kwani itawapa mwanga wa nini watapaswa kufanya katika mchezo huo


Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Mudathir Yahya amesema wachezaji wote wamejiandaa na mchezo huo na wako tayari kupambana


"Wachezaji wote tumejiandaa vyema kupigania alama tatu. Hakuna presha yoyote tumejipanga na tutapambania ushindi," alisema MudathirDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz