Yanga yatangaza viingilio mechi ya Rivers United - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yatangaza viingilio mechi ya Rivers United

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Yanga leo imetangaza viingilio vya mchezo wa mkondo wa pili robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United ambao utapigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wametangaza viingilio mapema ili kuwapa nafasi mashabiki kuwa na muda wa kutosha kununua tiketi kuepuka changamoto zinazojitokeza siku ya mchezo


Aidha Kamwe amewataka mashabiki kujenga utamaduni wa kununua tiketi zao mapema na sio kusubiri siku ya mchezo na hivyo kukumbana na changamoto zisizotarajiwa


"Tiketi zimeanza kuuzwa mapema ili kuhakikisha mashabiki wananunua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu ambao hujitokeza siku ya mchezo"


"Ni vyema tukaacha mazoea, tujenge utamaduni wa kununua tiketi mapema ili kuondokana na kadhia za dakika za lala salama," alisema Kamwe


Viingilio vya mchezo huo;


VIP A - Tsh 30,000/-


VIP B - Tsh 20,000/-


VIP C - Tsh 15,000/- 


Orange - Tsh 10,000/-


Mzunguuko - Tsh 5,000/-Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz