Yanga kutumia dakika 180 uwanja wa Liti, Singida - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kutumia dakika 180 uwanja wa Liti, Singida

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mchezo wa ligi kuu kati ya Singida BS dhidi ya Yanga ambao uliahirishwa kutokana na ushiriki wa Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC), sasa utapigwa May 04 katika uwanja Liti, Singida


Wananchi watalazimika kuweka kambi huko Singida kwani baada ya mchezo huo, siku tatu baadae watarudi tena uwanja wa LITI kuumana na Singida BS katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao utapigwa May 07


Zitakuwa dakika 180 za mapambano kwa Yanga ikihitaji kushinda mechi zote mbili


Yanga inahitaji kutetea ubingwa wa ligi kuu, ushindi dhidi ya Singida BS utawasogeza karibu zaidi kufikia malengo kwani wanahitaji alama nane kutoka mechi nne zilizobaki


Ili kutetea kombe la FA Yanga lazima ishinde dhidi ya Singida BS kutinga fainali zaidi Wananchi wanaomba watani zao Simba washinde dhidi ya Azam Fc ili 'kipigwe' tena derby katika FADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz