Walicho kisema wachezaji na viongozi wa Yanga baada ya kupangwa na Rivers United - EDUSPORTSTZ

Latest

Walicho kisema wachezaji na viongozi wa Yanga baada ya kupangwa na Rivers United

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wamefurahia droo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo watacheza na Rivers United ya Nigeria


Droo hiyo iliyofanyika Cairo, Misri Jumatano usiku, iliwashuhudia Wananchi wakipewa Rivers United, wapinzani ambao sio wageni kwao


Ilikuwa msimu uliopita katika mechi za awali ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga ilikabiliana na Rivers United na kupoteza mechi zote mbili nyumbani na ugenini kwa bao 1-0 na kujikuta wakiondoshwa katika michuano hiyo


Injinia Hersi amesema wanakumbuka matokeo hayo na sasa ni zamu yao kuwaadhibu mabingwa hao wa Nigeria


"Sisi tumefurahi kukutana na Rivers United, hii ni mechi ya kisasi kwetu kama ilivyokuwa mechi dhidi ya US Monastir. Tunasema hivi tutaenda kuwapiga Rivers United nje-ndani na kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho"


"Tulipokutana nao miaka miwili nyuma walitufunga mechi zote, hata hivyo hatukuwa katika ubora tulionao sasa. Tuliwakosa baadhi ya wachezaji wetu muhimu kutokana na vibali lakini kwa sasa tuko katika kiwango bora, tumaani uwezo wetu," alisema Hersi


"Baada ya droo hii nilizungumza na wachezaji, wamefurahi kwani ni mechi waliyoihitaji sana. Mayele aliniambia anawatamani kwelikweli Rivers United" 

Naye Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema droo hiyo imewapa nafasi nzuri ya kusonga mbele katika kombe la Shirikisho


"Droo hii ni nzuri kwetu, kwa ubora wa timu yetu nafikiri tunayo nafasi ya kufanya vizuri na kusonga mbele katika michuano hii," alisema Kaze


Mechi ya kwanza ya robo fainali itapigwa Nigeria April 23 na mchezo wa marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa April 30


KISASI NI HAKI...!



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz