Wababe wanne waliotinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Wababe wanne waliotinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mechi mbili za robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika zilihitimishwa usiku wa kuamkia leo kwa mabingwa wa kihistoria Al Ahly kukata tiketi kibabe baada ya kulazmisha suluhu ya bila kufungana nchini Morocco dhidi ya Raja Casablanca


Al Ahly walishinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa huko Misri


Al Ahly iliungana na Esperance ya Tunisia ambayo pia ilitinga nusu fainali licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JS Kbalylie


Esperance ilishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Algeria


Mapema jana Mamelodi Sundowns ilitinga nusu fainali kibabe kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2 dhidi ya CR Belouizdad


Mamelod walishinda mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa pili wakiongezea juu ya ushindi wao wa mabao 4-1 katika mchezo mkondo wa kwanza


Al Ahly, Mamelod na Esperance zimeungana na Wydad Athletic ambayo ilitangulia nusu fainali juzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Simba ya Tanzania baada ya marokeo ya sare ya bao 1-1 katika mechi zote mbili za robo fainali


Al Ahly itachuana na Esperance hatua ya nusu fainali wakati Mamelodi watachuana na wydad AthleticDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz