Ni leo Yanga vs Rivers united Kisasi lazima kilipwe - EDUSPORTSTZ

Latest

Ni leo Yanga vs Rivers united Kisasi lazima kilipwe

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Leeeo ndio leoooooo..leo ni kivumbi na jashoooo...! Ndivyo Wananchi watakavyokuwa wakiimba majukwaani jioni ya leo watakapokuwa wakiwakabili Rivers United katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika


Yanga itaingia katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 1 usiku ikiwa na mtaji wa mabao 2-0 ushindi waliopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa huko UYO, Nigeria


Jukumu la Wachezaji wa Yanga ni moja tu, kusaka ushindi ambao utawahakikishia kutinga nusu fainali ya michuano hiyo na kuweka rekodi kwa klabu za Tanzania katika mashindano ya CAF


Tangu michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho ilipoanzishwa na CAF, hakuna timu ya Tanzania iliyowahi kutinga nusu fainali


Rivers United wako nchini tangu juzi na jana walikamilisha mazoezi yao katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Yapo maigizo wanafanya kujaribu kuwaondoa Yanga  mchezoni jana usiku wakiibua taarifa kuwa basi lao limevunjwa na kupuliziwa dawa pamoja na kuibiwa pesa wakati wakifanya mazoezi yao ya mwisho


Walianza kwa kusema hawana hela hivyo watachelewa kuja nchini lakini leo wanasema wameibiwa hela walizoacha kwenye basi wakati wakienda mazoezini ...!


Bila shaka wanafahamu nafasi yao ya kuifunga Yanga ni ndogo, wanajaribu kutengeneza mazingira ili wakifungwa ionekane kulikuwa na sababu


Hata hivyo vijana wa kocha Nasreddine Nabi hawapaswi kusikiliza sarakasi hizi za wapinzani wao, wafahamu watakuwa na dakika 90 ngumu uwanja wa Benjamin Mkapa leo


Watahitaji kupambana ili kuhakikisha wanapata ushindi ambao utawapeleka nusu fainali na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya klabu ya YangaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz