Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema wamejiandaa kuwashangaza Wydad Athletic katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Simba itakuwa ugenini siku ya Ijumaa, April 28 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Mohammed V, saa 3 usiku kwa saa za Tanzania
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Robertinho alisema amekiandaa kikosi chake kimbinu kukabiliana na Wydad katika mchezo muhimu wa kuwania tiketi ya kutinga nusu fainali
"Tutawashangaza wapinzani wetu kwa sababu tumefanya kazi kubwa kufika hapa tulipo, tumekuwa tukibadili mazoezi kulingana na mpinzani tunayekutana nae"
"Binafsi ningependa tushinde magoli mawili au matatu lakini hata goli moja litatufaa kutokana na kile tulichokipata kwenye mchezo wa kwanza"
"Nina imani kubwa na wachezaji wangu na viongozi kwa ujumla, tumejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huu. Tumekuwa na mfululizo wa matokeo mazuri, hili ni jambo muhimu kwetu," alisema Robertinho
Nae kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho alisema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo, wamefanya maandalizi kabamba kuhakikisha wanashinda
Sakho amesema hawana hofu na mashabiki wa Wydad zaidi vurugu zao zitawaongezea ari ya kupambana
No comments:
Post a Comment