Timu ambazo Yanga atakutana nazo Robo fainali kombe la shirikisho hizi hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Timu ambazo Yanga atakutana nazo Robo fainali kombe la shirikisho hizi hapa

 

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Baada ya Yanga kuizamisha TP Mazembe kwenye dimba lao la nyumbani huko DR Congo kwa kuwachapa bao 1-0, US Monastir walipaswa kushinda angalau mabao matatu dhidi ya Real Bamako ili kuweza kuiondosha Yanga kileleni mwa kundi D


HAIKUWEZEKANA kwani Monastir walipata ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kuihakikishia Yanga kumaliza kileleni mwa kundi  wakiwa na alama 13


Yanga sasa itakuwa na faida kwenye hatua ya robo fainali kwa kuanzia ugenini na kumalizia mechi ya pili nyumbani


Yanga, AS FAR, Malumo Galants na ASEC Mimosas zimemaliza vinara wa makundi wakati US Monastir, Rivers United, USM Alger na Pyramids zimemaliza katika nafasi ya pili


Katika hatua ya robo fainali Yanga itamenyana na kati ya Rivers United, USM Alger au Pyramids


Droo ya mechi za robo fainali itafanyika siku ya JumatanoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz