Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumapili - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumapili

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, 35, hatapunguza malipo yake ili kusalia Paris St-Germain . (Goal)


Messi ana maamuzi ya kufanya iwapo ataondoka kutoka mabingwa hao wa Ufaransa, na huenda akachukua ofa kutoka kwa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia au kurejea Barcelona. (Mirror)


Manchester City na Real Madrid wamemfanya mlinzi wa RB Leipzig mwenye umri wa miaka 21 wa Croatia Josko Gvardiol kuwa mlengwa wao wa kati, na timu hiyo ya Ujerumani ingetaka pauni milioni 75. (90min)


Liverpool na Manchester City wote wanafanya kazi ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 24, kutoka Chelsea msimu huu wa joto, huku Reds kwa sasa wakionekana kuwa mstari wa mbele. (Football Insider)


Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amemwambia meneja wa zamani Mauricio Pochettino hataki Muargentina huyo kurejea katika klabu hiyo wakati wa mazungumzo kuhusu uwezekano wa kurejea. (Star)


Mshambulizi Mfaransa h, 27, ni miongoni mwa wachezaji wanane ambao Manchester United wanatazamia kuwauza msimu huu wa joto. (Football Insider) Chelsea wanakabiliwa na uwezekano wa kuwalipa wachezaji mamilioni ya pesa ili kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto huku wakipania kupunguza dau lao la mishahara. (Sun)


Manchester United wanafuatilia hali ya mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 23, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Chelsea. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)


United inamshabikia mlinda lango wa Porto Mreno Diogo Costa, 23, na Mhispania David Raya, 27, wa Brentford - hata hivyo hakuna ambaye hatataka kuhama ikiwa mchezaji nambari moja wa klabu hiyo David de Gea, 32, atatia saini mkataba mpya. (Express)


Meneja wa Italia Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa Brazil wanataka kumteua kama kocha wao, hata hivyo anataka kusalia Real Madrid. (ESPN)


Matumaini ya Aston Villa kumsajili kiungo wa kati wa Hispania Oihan Sancet kutoka Athletic Bilbao yamepata pigo baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kusaini mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu hiyo ya La Liga. (TeamTalk)


Tottenham na PSG wamepewa fursa ya kumsajili beki wa Hispania Aymeric Laporte, 28, kutoka Manchester City. (90 Minutes)


Manchester City inalenga kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ansu Fati kufuatia maoni yaliyotolewa na babake fowadi huyo kuhusu kukosa muda wa kucheza. (Football Insider)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz