Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumanne - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumanne

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice angependelea kuhamia Arsenal katika msimu ujao wa joto, huku Newcastle pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (TalkSPORT)


Rice ni miongoni mwa wachezaji waingereza, ikiwa ni pamoja na kiungo wa Leicester City James Maddison, 26, na mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 27, wanaosakwa na Magpies wakitaka kusajili wachezaji wakubwa na wakali wanne msimu huu. (Telegraph)


Barcelona wana uhakika wa kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, kwa uhamisho huru mara tu mkataba wake na timu hiyo ya ligi kuu England utakapokamilika msimu wa joto. (Times)


Tottenham iko mbioni kuchuana na Chelsea katika mbio za kumnasa meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique. (Telegraph)


Kocha wa zamani wa Spurs Antonio Conte huenda akajiunga na Roma msimu ujao, huku meneja wao wa sasa Jose Mourinho huenda akuchukua mikoba ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa. (CalcioMercato via Mirror)


Aston Villa, Everton na West Ham wote wanavutiwa na mshambuliaji wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 28 Joaquin Correa. (Sport Witness)


Chelsea itajaribu kumuuza Conor Gallagher msimu huu wa joto kwenda vilabu kadhaa vya Ligi kuu ya England na Ulaya vinavyomtaka kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 23. (Mail)


Arsenal wamempa Reiss Nelson, 23, mkataba mpya lakini bado kuna shaka juu ya mustakabali wake wa muda mrefu, huku Aston Villa, Fulham, West Ham na Brighton wakiwa miongoni mwa timu zinazowania kumsajili winga huyo wa England. (Mail)


West Ham wanatazamiwa kupokea ada ya takriban £1.75m kutoka kwa klabu ya Uturuki ya Besiktas kwa ajili ya beki wake wa kushoto wa DR Congo Arthur Masuaku, 29, baada ya kipengele cha wajibu wa kumnunua kuafikiwa. (Football Insider)


Aston Villa wameweka nia ya kutaka kumnunua beki wa kulia wa Manchester City na England Kyle Walker, 32, ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto wa 2024. (Football Insider)


Chelsea wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa Colombia Kendry Paez, 15, ambaye atajiunga na klabu hiyo mwaka 2025 akiwa na umri wa miaka 18, kwa mkataba wa thamani ya euro 20m (£17.66m). (Fabrizio Romano)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz