Tetesi za usajili barani ulaya Leo Alhamisi - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Alhamisi

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Manchester City wanaongoza Real Madrid katika kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham baada ya Liverpool kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 19. (ESPN)


Mchezaji wa West Ham na Muingereza Declan Rice, 24, mchezaji wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21 Moises Caicedo, nyota wa Inter Milan na Italia Nicolo Barella, 26, na mchezaji wa Wolves na Ureno Matheus Nunes, 24, wamesalia kwenye orodha ya Liverpool inayomsaka kiungo mpya. (Florian Plettenberg)


Barcelona itazidisha hamu yao kumnunua Ilkay Gundogan baada ya kufurahishwa na mchezo wa kiungo huyo wa kati Mjerumani mwenye umri wa miaka 32 akiwa na Manchester City dhidi ya Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa. (Sport - kwa Kihispania)


Arsenal, Liverpool na Manchester United wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 20. (Footmercato - kwa Kifaransa)


Tottenham, West Ham na Crystal Palace wote wanamtaka meneja Mholanzi Arne Slot, ambaye ameigeuza Feyenoord kuwa viongozi wa ligi ya Eredivisie. (Times- usajili unahitajika)


Arsenal wanalenga kumnunua winga wa Crystal Palace na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 th msimu wa joto, huku mchezaji huyo akiwa na thamani ya zaidi ya £40m. (Football Transfers)


Fulham, Aston Villa na Crystal Palace wanavutiwa na kiungo wa kati wa Besiktas na Ureno Gedson Fernandes, 24. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)


Liverpool wametuma maskauti kumwangalia kiungo wa kati wa Fulham Joao Palhinha mara kadhaa wakifikiria kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 27 msimu wa joto. (Football Insider)


Timu ya wanawake ya Barcelona itajaribu tena kumsajili mshambuliaji wa Lyon na Norway Ada Hegerberg, huku timu hiyo ya Uhispania ikiwa tayari kutoa ada ya kuvunja rekodi ya dunia ya £420,000 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (90min)


Arsenal, Bayern Munich, Borussia Dortmund na Monaco wameonyesha nia ya kumnunua fowadi wa Crystal Palace na Ivory Coast h, 30, huku kandarasi yake ikikamilika msimu wa joto. (Footmercato - kwa Kifaransa)


Beki wa zamani wa Uingereza Chris Smalling, 33, atasaini mkataba mpya wa miaka miwili katika klabu ya Roma wiki hii licha ya nia ya kutakiwa na Inter Milan, Juventus na klabu kadhaa za Premier League. (i Sport)


Arsenal itadai pauni milioni 35 kwa mshambuliaji wa Uingereza Folarin Balogun, 21 ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo huko Reims na analengwa na RB Leipzig. (Florian Plettenberg)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz