Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumatatu - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumatatu

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Tottenham wameonesha nia ya kumsajili winga wa Morocco Hakim Ziyech, 30, kutoka Chelsea msimu huu wa joto. (Football Insider)


Kocha wa zamani wa Leeds Jesse Marsch ameamua kutochukua kazi ya Leicester City licha ya kukaribia kufikia makubaliano ya mwisho (Telegraph - subscription required)


AC Milan wamemuongeza mshambuliaji wa England chini ya miaka 21 Folarin Balogun, ambaye yuko kwa mkopo Reims kutoka Arsenal , kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa katika majira ya joto, ingawa wanatarajia The Gunners kuomba zaidi ya euro 30m (£26.5m) Calciomercato - kwa kiitalia)


Manchester United pia imewaweka kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, na kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 24, kwenye orodha yao fupi ya uhamisho. (Telegraph -usajili unahitajika)


Mshambulizi wa zamani wa Ufaransa Karim Benzema, 35, anataka kusalia Real Madrid kwa angalau msimu mmoja zaidi baada ya kukataa ofa kutoka Saudi Arabia. (Marca kwa Kihispania)


Chelsea na Liverpool wanakaribia kumlenga Nicolo Barella wa Inter Milan , huku miamba hao wa Italia wakiwa tayari kumuuza kiungo huyo wa kati wa Italia, 26, kwa £44m. (Clciomercato, kupitia Sun)


Manchester United imekuwa na mazungumzo chanya na Monaco kuhusu uwezekano wa kumsajili mlinzi wa Ufaransa Axel Disasi, 25. (Give Me Sport)


Manchester United wanaweza kuelekeza nguvu zao katika kumsajili mlinzi wa Bayern Munich Mfaransa Benjamin Pavard, 27, ikiwa miamba hao wa Ujerumani wataishinda United katika kumsajili mlinzi wa Bayer Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong, 22, msimu huu. (Football Insider)


Kipa wa Uhispania David Raya hatasaini mkataba mpya katika klabu ya Brentford , ambao wanatazamiwa kuomba ada ya euro 40m (£35.4m) kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu huu. (Fabrizio Romano)


Bologna wanapambana na Leicester City kumsajili kiungo wa kati wa Birmingham City wa Wales h, 18. (Sun)


Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, anasema bado anasubiri kujadili iwapo atasaini mkataba mpya na Juventus . Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kuisha msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)


Mchezaji wa Borussia Dortmund Marco Reus, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika msimu huu wa joto, anatazamiwa kusaini mkataba mpya msimu ujao, ingawa winga huyo wa Ujerumani, 33, atalazimika kuzungumza kukatwa mshahara. (Bild - kwa Kijerumani)


Kocha Xavi Hernandez atasisitiza kwamba Sergio Busquets abaki na Barcelona kwa angalau msimu mmoja zaidi kabla ya kiungo huyo wa zamani wa Uhispania, 34, kuondoka na kujiunga na klabu ya MLS. (Target)


Real Madrid ilijaribu kumsajili bosi wa muda wa Chelsea Frank Lampard mara mbili wakati kiungo huyo wa zamani wa England, 44, alipokuwa mchezaji muhimu wa The Blues - mwaka 2005 na 2010. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz