Taarifa Mpya kuhusu kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa Mpya kuhusu kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote akitokea Ubelgiji ambako alikwenda kuhuisha hati yake ya kusafiria


Yanga inakabiliwa na mechi mbili za Ligi Kuu kabla ya kuwakabili Rivers United kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika utakaopigwa April 23 huko Nigeria


Keshokutwa Jumanne April 11 Yanga itaikaribisha Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Azam Complex


Jumapili April 16 mchezo wa pili dhidi ya Simba utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa. Hizi ni mechi mbili muhimu ambazo Yanga inahitaji kushinda ili kurahisisha mbio zake kuelekea ubingwa wa 29


Nabi alilazimika kusafiri Ubelgiji kuhuisha hati yake ya kusafiria akikosa safari ya Yanga DR Congo kuhitimisha hatua ya makundi ya Shirikisho dhidi ya TP Mazembe


Amekosa mechi mbili, mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold ukiwa wa pili Yanga ikitinga nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz