Kmc waahidiwa Kila Goli laki 5 - EDUSPORTSTZ

Latest

Kmc waahidiwa Kila Goli laki 5

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mdhamini Mkuu wa KMC fc inayoshiriki Ligi kuu ya NBC Meridian Bet wameahidi kutoa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa kila goli ambalo klabu hiyo itapata katika michezo ya ligi kuu iliyosalia


Lengo ni kutoa motisha kwa wachezaji kupambana zaidi na kukwepa mkasa wa kushuka daraja


Akizungumza na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo ya Meridian bet Bw. Matina Nkurlu, alisema kwamba lengo la zawadi hiyo ni kutoa motisha ili kuweza kuiweka timu kwenye mikono salama mpaka mwisho wa msimu


"Tumeamua kununua kila goli mtakalofunga kwa Tsh Laki Tano kwenye michezo yenu ya Ligi Kuu iliyosalia. Lakini jambo kubwa zaidi kiasi kitakacho patikana kitatumika kurejesha kwa jamii kwa sababu KMC ni timu ya Wanakinondoni na Watanzania wote," alisema


Kwa upande wa Nahodha wa KMC FC Emmanuel Nvuyekule alipongeza juhudi za Mdhamini wao na kuahidi kupambana zaidi


"Nimshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwepo nanyi na kuzipokea taarifa hizi, lakini pia niwashukuru kwa kuja na wazo hili naamini hii itaongeza hamasa na kujituma kwenye timu yetu"


"Kubwa zaidi ni kwamba tuna muahidi mdhamini wetu kuwa tutafanya vizuri na tutafunga magoli mengi sana ili kusaidia jamii kwa wingi zaidi"


KMC imecheza michezo 25, imebakiza michezo 5 mkononi kabla ya Ligi kumalizika. Kwenye msimamo wanashika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 26, Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Geita Gold.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz