"Nimesikia Wydad wameuza tiketi zote, tunaenda kuwapiga mbele za mashabiki zao" Ahmed Ally - EDUSPORTSTZ

Latest

"Nimesikia Wydad wameuza tiketi zote, tunaenda kuwapiga mbele za mashabiki zao" Ahmed Ally

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Wydad Athletic watarajie kukutana na timu tofuati kabisa na zile walizowahi kucheza nao katika uwanja wao wa nyumbani Mohammed V


Kikosi cha Simba kiko nchini Morocco kuelekea mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad ambao utapigwa Ijumaa, April 28 saa nne usiku


Akiwa miongoni mwa msafara wa pili wa viongozi ulioondoka Dar jana jioni kuelekea Morocco, Ahmed alisema wanakwenda Morocco kuandika historia ya kufuzu nusu fainali ya ligi ya mabingwa


Ahmed amesema Simba ina malengo makubwa kwenye michuano hiyo, Wydad watarajie kukumbana na wakati mgumu hapo hapo kwenye uwanja wao


"Tunawaheshimu Wydad, ni timu kubwa  na mabingwa watetezi wa michuano hii lakini tunawaambia hatuwaogopi, tunakwenda Morocco tukiwa na malengo ya kufuzu nusu fainali"


"Nimesikia wameuza tiketi zote za mchezo, mimi nasema sisi tumefurahi kwani tunakwenda kuwaadhibu mbele ya mashabiki wao. Waombolezaji hata walie vipi kwenye msiba hawawezi kuamsha maiti," alitamba Ahmed


Simba itahitaji ushindi au hata matokeo ya sare siku ya Ijumaa ili kujihakikishia tiketi ya kucheza nusu fainali


Ikitokea imepoteza isiwe zaidi ya tofauti ya bao moja na iwapo Simba itafunga bao ugenini basi itatinga nusu fainali



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz